Mtekinolojia wa maabara ya hospitali ya rufaa wa mkoa Iringa Bw. Amulike Mwalongo amesema, hali hiyo imetokana na wananchi kukosa kuchangia damu, ukosefu wa vifaa vya kutolea damu na ukosefu wa fedha.
Bw. Mwalongo amesema, tokea Disemba mwaka jana hospitali hiyo haijapata damu kutoka benki ya damu ya mkoani Mbeya kwani hakuna damu ya kutosha.
Naye Afisa ubora wa viwango vya maabara Bibi Emmy Mkupasya amesema, ukosefu wa uelewa wa wananchi juu ya uchangiaji wa damu kumepelekea kuiachia serikali kwa imani ndiyo yenye jukumu hilo.
Bibi Emmy amewaasa wananchi kuendelea kujitolea damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye matatizo hayo kwani kwa sasa wanafunzi wachache wa shule na vyuo wanafanya hivyo.
Hata hivyo, ameshauri wanawake wajawazito kwenda kliniki kupima afya zao ili wanapogundulika kuwa watajifungua kwa upasuaji waweze kuwachangiwa damu mapema.