
Akiongea jijini Dar es Salaam wakati akizindua vitabu vya uchambuzi wa matokeo ya kuhitimu elimu ya sekondari 2013,Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt.Charles Msonde amesema somo lenye kiwango cha juu ni Kiswahili pekee hivyo juhudi za pamoja katika kupandisha kiwango cha ufaulu zinahitajika.
Akizindua vitabu hivyo, Naibu Waziri wa wizara Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini, Mhe. Jenister Mhagama amesema serikali inaendelea kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuajiri walimu wapya, ambapo mwaka huu serikali imeajiri jumla ya walimu 18,093 wa shule za sekondari wakiwemo 5,416 wenye elimu ya Stashahada na 12,677 wenye Shahada.