Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Haki elimu, (katikati) Godfrey Boniventura akiongea na Waandishi wa Habari hawapo pichani.
Aidha, shirika hilo limesema kuchelewa au kutopelekwa kwa pesa za ruzuku kwa kiasi fulani kumechangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hakielimu, Godfrey Boniventura amesema hali hiyo imebainika kufuatia ufuatiliaji uliofanywa na shirika hilo katika mikoa na wilaya kadhaa nchini ambapo kwa wastani shule mpaka sasa zimepokea shilingi zisizozidi elfu nane, kati ya shilingi elfu kumi anazostahili kupata kila mwanafunzi, kiwango ambacho ni sawa na asilimia tisa tu ya pesa yote.
Ameongeza kuwa Ruzuku ya Mwanafunzi ndio pesa zinazotogemewa na shule kwa ajili ya uendeshaji,hi inamaanisha kuwa shule nyingi sasa hivi zina uhaba wa fedha za uendeshaji na hivyo kuathir upatikanaji wa elimu bora mashuleni.
Bonaventura changamoto ya ukosefu wa fedha na hali hiyo inaathiri shule kupata mahitaji ya msingi kama chaki, vifaa vya ofisini na kukabili gharama ndogo za uendeshaji na hali hiy inakuja zikiwa imebaki miezi miwili kumaliza mwaka wa fedha wa 2014/2015