Friday , 31st Jul , 2015

Chama cha wataalam wa ustawi wa jamii Nchini (TASWO) kimeandaa kongamano la siku mbili mkoani Iringa ili kuunganisha nguvu ya pamoja juu ya haki za watu wenye ulemavu wa ngozi.

Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mapambano ya kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino),Said Ndonge

Katibu wa chama cha TASWO Bw. Nicolaus Mshana amesema lengo la kongamano hilo ni kupitia mifumo ya utendaji kwa makundi maalum ya watu wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.

Aidha Bw. Mshana amesema kongamano hilo pia litasaidia kujenga mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu na kuondoa hali ya unyanyapaa miongoni mwao.

Mkutano huo wa mwaka umeshirikisha mashirika yasiyo ya kiserikali, jeshi la polisi, maofisa wa ustawi wa jamii kutoka mikoa mbalimbali.