Tuesday , 12th Jul , 2016

Mbunge wa Mtwara vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewataka wazazi na walezi Mkoani Mtwara kutumia fursa inayotolewa na serikalya kutoa elimu bila malipo kwa kuwapeleka shule watoto wao, ili kuwajengea misingi bora ya maisha.

Mbunge wa Mtwara vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Hawa Ghasia.

Akizungumza baada ya kukabidhi madawati Mia mbili katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Mbunge huyo Mhe. Hawa Ghasia, amesema jukumu walilonalo wazazi kwa sasa ni kuwasimamia watoto wao kuhakikisha wanasoma kwa bidi.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Zacharia Nachoa, amesema kuwa halmashauri yake imekamilisha tatizo la madawati kwa shule za sekondari na kwa shule za msingi wanaelekea kukamilisha, huku mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Madimba Ahmad Kwerendu akishukuru kutokana kupatiwa mdawati hayo.

Madawati hayo yamegawanywa katika shule mbili za sekondari katika halmashauri hiyo ambazo ni sekondari ya Madimba na sekondari ya Kisiwa.

Sauti ya Mbunge wa Mtwara vijijini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Hawa Ghasia,