Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA (CRC) Bi. Gladness Munuo.
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA (CRC) Bi. Gladness Munuo, ameimbia East Africa Radio kuwa suala la maendeleo pamoja na uzingatiaji wa haki za binadamu ni la msingi hususani kipindi hiki ambacho wagombea wamekuwa wakiwania kuteuliwa kuongoza.
Bi. Munuo amesema kiongozi anatakiwa ni lazima ahakikishe sheria mbalimbali zinazowakandamiza wanawake zinafanyiwa kazi ikiwemo sheria ya Ndoa na Sheria ya Mirathi ambayo kina mama wengi sana wanateseka nayo.
Ameongeza kuwa kuna sheria ambazo mpaka sasa zina mifumo dume ambazo nyingi zinatokana na mila na desturi kwa hivyo zinatakiwa kurekebisha kama sio kufutwa kabisa na kutungwa mpya ili kuwalinda watoto na wanawake katika kunyanyaswa kijinsia.
Aidha, Bi Munuo amewataka Watanzania kuzingatia kwa umakini mkubwa kauli zinazotolewa na wanasiasa na kujiuliza iwapo ahadi wanazotoa kuhusu haki za binadamu zinatekelezeka, hususani kwa viongozi ambao waliwahi kuwa madarakani katika awamu zilizopita serikalini.