Thursday , 20th Sep , 2018

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjao Mh. Anna Mghwira, amesema pamoja na kupokea ugonjwa wa kipindupindu kutoka mkoani Manyara lakini wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira

Mh. Anna Mghwira ameyasema hayo leo Septemba 20, 2018, kwenye mahojiano na www.eatv.tv  ambapo mbali na kutaka kujua hali ilivyosasa, tulimuuliza juu ya chanzo cha ugonjwa huo ambapo ameibanisha kuwa ulianzia Manyara.

''Wilaya ya Moshi vijijini imepakana na Manyara ambapo ugonjwa huo ulianzia huko, lakini sisi tulifanya taratibu zote kuhakikisha tunadhibiti ka kupeleka watalaam hivyo wagonjwa wote wakawa wanatibiwa Moshi vijijini kwa ushirikiano na mkoa wa Manyara'', amesema. 

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema wameshaweka tahadhari katika maeneo hatarishi hususani yale yaliyopo kandokando ya mto Pangani katika wilaya za Arumeru, Hai, Mwanga, Same, Korogwe na Pangani yenyewe.

Kuhusu usalama wa abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali ambao mabasi yao huingia katika kituo cha mabasi cha Moshi mjini, Mghwira amesema wameshatoa tahadhari kwa viongozi wa idara husika kuhakikisha vyakula na vinywaji vinauzwa katika mazingira salama.

Hadi sasa katika wagonjwa 29 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya TPC, 28 kati yao wametumia dawa na kuruhusiwa hivyo hadi leo Septemba 20, 2018 kuna mgonjwa mmoja tu ambaye bado amelazwa.

Zaidi msikilize Mh. Mghwira akifafanua zaidi hapa chini.