Naibu Waziri ofisi ya Rais ,Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo,
Agizo hilo limetolewa leo na Naibu Waziri ofisi ya Rais ,Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo, wakati akikagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa halmashauri ya wilaya ya Chamwino ya kuhakikisha Soko la Buigiri lilojengwa tangu mwaka 2003 kutumika.
Jafo amesema pamoja na kutekelezwa kwa agizo hilo ni lazima Soko hilo lisimamiwe ili lifanye kazi muda wote.
Ameiagiza halmashauri kuhakikisha wafanyabiashara wa Soko hilo wanapewa kipaumbele cha kupatiwa mikopo ili waweze kuimarisha biashara zao.
"Inapowekwa miundombinu ya aina hii inatakiwa ifanye kazi kwani dhamira ya serikali ni kuhakikisha kila mmoja anafanya kazi ili kuondokana na umaskini...Vijana wekeni majiko ya nyama hapa, ili kufanya watu waweze kusimama kununua bidhaa mbalimbali,"amesema Jafo.
Awali akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa agizo hilo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Saada Mwaluka, amesema baada ya kutolewa maagizo hayo waliunda kikosi Kazi cha kuhakikisha Soko hilo linaanza kufanya kazi.
Amesema kwa sasa Soko limeanza kufanya kazi lakini Changamoto iliyopo ni watu kupungua siku hadi siku kutokana na ukosefu wa mitaji ya kuendeshea biashara zao.
"Wilaya tumejipanga kuhakikisha Soko linafanya kazi vizuri na tumewasiliana na wasindikaji mafuta ya alizeti walete bidhaa zao katika Soko hili ili kufanya kuwepo na mzunguko mkubwa wa biashara,"amesema Mwaluka.