Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mtwara katika uzinduzi rasmi wa mafunzo ya programu ya kijana jiajiri, iliyofanyika katika ukumbi wa Veta, Mtwara, mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, amesema vijana kati ya miaka 15-35 wanaajirika katika sekta rasmi kwa kiwango kisichozidi asilimia moja.
Bi. Fatma amesema takwimu za mwaka zinaonyesha Tanzania ina takribani vijana milioni 15.5 swa na asilimia 34.7 ya watu wote nchini lakini wengi hawana ajira kutokana na fursa chache kidogo kulinganisha na idadi halisi ya vijana
Kwa upande wake, mshiriki wa mafunzo hayo, Dadi Namtema, amesema kupatiwa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji, ni jambo la msingi kwao kutokana na vijana wengi kuwa tegemezi na kujikuta wakiishi maisha yasio na muelekeo mpaka umri unawaacha.