Wednesday , 27th May , 2015

Katibu mkuu wa chama cha Albino Tanzania Bi Ziada Nsembo ameitaka serikali kutumia teknolojia ya kisasa katika vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Chama cha Albino Tanzania Bi Ziada Nsembo.

Akizungumza na East Africa Radio Bi Ziada amesema kutokana na ucheleweshwaji wa kesi za maalbino, matumizi ya teknolojia yataharakisha masuala ya ushahidi kwa kiasi kikubwa kwani mpaka sasa kesi nyingi zinacheleweshwa kutokana na ushahidi kutokidhi matakwa ya sheria.

Bi. ziada amesema kuwa teknolojia hiyo haitakuwa na ubabaishaji na ushahidi kutokana na sasa mtu anaweza kushikwa na kithibitisho ikiwemo panga lenye damu lakini bado mahakama inasema hakuna ushahidi wa kwa hiyo teknolojiaq hiyo hiyo inaweza kudhibiti hali hiyo.

Amesema kuwa pia suala la teknolojia litaepusha kwa kiasi kikubwa kesi kuamuliwa kwa Rushwa na pia amesema wameamua kushirikisha na nchi nyingine kimataifa ili kusaidia upepelezi kutokana na kutoka kuwa na imani na serikali jinsi inavyoshughulikia suala hilo.

Pia ziada amemtaka Rais aweke saini ili kunyongwa kwa watu ambao wamehukumiwa kutokana na kesi hizo kwa kuwa mpaka sasa hawaamini hukumu zinazotolewa na mahakama za Tanzania na kusema tangu mwaka 2010 hakuna hata mtu mmoja angekuwa ameshanyongwa.

Aidha kuelekea siku ya Kimataifa ya Albinism Nchini Tanzania, Bi .Ziada ametoa pendekezo la kutaka Kesi zote zinazohuzu watu wenye ulemavu wa ngozi kusikilizwa na kutolewa hukumu katika Mahakama ya Afrika Mashariki.