Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi za Takwimu nchini Tanzania Bw. Moris Oyuke (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hivi karibuni.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi za Takwimu nchini Tanzania Bw. Moris Oyuke amesema ukuaji huo wa pato la taifa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na sekta ya Madini, umeme pamoja na kilimo.
Kwa mujibu wa Oyuke, Kenya ambayo inatajwa kuwa na uchumi mkubwa safari hii pato lake limepungua kidogo na kushika nafasi ya pili na kwamba nchi zinazofuatia kwa pato lake kufanya vizuri ni Uganda, Rwanda na ya mwisho Burundi.
Kwa upande wa Tanzania, Bw. Oyuke ametaja sekta zilizochangia ukuaji wa pato hilo kuwa ni za madini, umeme pamoja na kilimo.