Thursday , 15th Oct , 2015

Wataalam wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA, wamesema kuwa kamisheni ya nishati ya atomiki nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto kadhaa katika kujenga chombo cha kudhibiti nyuklia.

Moja ya vinu vya kudhibiti Nykulia vilivyopo nchini Japan,

Wataalam hao wa timu ya kutathmini udhibiti wa nyuklia, wamesema hayo wakihitimisha ziara ya siku kumi nchini Tanzania kutathmini mkakati wa udhibiti wa nyuklia na usalama wa mnururisho wa mionzi ya nyuklia.

Kiongozi wa timu hiyo, Tom Ryan, amesema ingawa Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi, kuna fursa nyingi pia katika changamoto hizo, akiongeza kuwa serikali ikijituma na kukabiliana na changamoto hizo, chombo kinachodhibiti nishati ya nyuklia nchini humo kina fursa ya kuwa huru, imara, na chenye kuweza kutenda kazi ipasavyo.

Tanzania haina vinu vya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme au utafiti, ingawa hutumia mnururisho katika matibabu na usindikaji na inapanga kuanzisha uchimbaji madini ya ureni.