
Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya Ifakara health Institute (IHI) Dkt Salim Abdullah.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dkt. Salim Abdullah amewaambia wandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa utafiti huo unafanywa nchini baada ya kuonyesha mafanikio nchini Marekani ambapo watu wote sita waliofanyiwa majaribio ya kinga hiyo hawakuweza kuugua ugonjwa wa malaria.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa taasisi ya afya na magonjwa yanayozikumba nchi za ukanda wa joto ya Swiss Tropical and Public Health Institute yenye makao yake makuu nchini Uswisi, Profesa Marcel Tanner amesema iwapo itathibitishwa na kuonyesha mafanikio, kinga hiyo itafanikisha juhudi za kuutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria.