Wednesday , 7th Dec , 2016

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imeeleza kuwa kushindwa kuwekeza kikamilifu katika sekta ya ufugaji nchini kutapelekea sekta hiyo kushindwa kuondoa umasikini, uhaba wa chakula, kukuza uchumi na kuchochea uendelezwaji wa viwanda.

Ng'ombe

Mchumi Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Stephen Michael amesema, tafiti zilizofanywa na taasisi za kimataifa kwa kushirikiana na wizara hiyo zinaonesha kuwa miaka 15 ijayo Tanzania itakuwa na uhaba wa mazao yatokanayo na ufugaji ikiwa ni pamoja na Maziwa, Nyama na Ngozi hivyo kupanga njia madhubuti za kupambana na changamoto zote katika sekta hiyo kunapaswa kutiliwa mkazo.

Aidha. Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Magembe Makoye amesema bila serikali kutekeleza sheria inayoainisha kutengwa kwa maeneo ya ufugaji na kuruhusu wafugaji kuyatumia hakuna mbinu itakayopelekea ufugaji kuchangia kikamilifu katika uzalishaji wa chakula na uchumi.