Wednesday , 23rd Apr , 2014

Taasisi ya saratani nchini Tanzania imesema kuwa serikali haina uwezo wa kuwapa tiba watoto zaidi ya 2000 ambao wanabainika kuugua ugonjwa wa saratani kote nchini Tanzania kila mwaka.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya saratani ya Ocean Road.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya saratani ya Ocean Road nchini Tanzania, Prof Twalib Ngoma, ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kwamba kati ya watoto hao serikali inauwezo wa kutibu watoto wasiozidi 400 tu.

Profesa Ngoma amesema taifa linaweza kuepuka vifo vya watoto vinavyotokana na kukosa matibabu ya saratani kwa kujitolea kuchangia gharama za matibabu kwa watoto, ambao amedai kuwa ni robo ya zile zinazotumika kwa mtu mzima.