
Dkt. Charles Tizeba
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo katika Ghala Kuu la Mbolea, Meneja wa Kampuni ya serikali ya kuzalisha mbolea nchini-TFC, Salum Mkumba amesema kuwa katika wiki mbili zijazo maeneo yote yaliyopangiwa na wizara kupata mbolea hiyo ambayo ni ya ruzuku yatakuwa yameshapata mbolea hizo ambazo zitapekelewa kwenye uongozi wa kijiji kwa ajili ya kuwagawia wahusika.
Amebainisha kuwa mpaka sasa zoezi la usambazaji wa mbolea hizo limeshaanza hivyo amewataka wakulima wote nchini kujiandaa kuzipokea kwa ajili ya kurutubisha mimiea yao ambapo kwa siku wanatarajia kusambaza Tani 700 hadi 900 kwa siku.
Naye Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Pembejeo kutoka Wizara ya Kilimo, Miguo na Ufugaji Shenali Nyoni ameeleza kuwa mbolea hiyo itapelekwa hasa kwenye maeneo yanayozalisha mazao ya mahindi na mpunga kwa kiasi kikubwa hasa mikoa ya nyanda za juu kusini.