Mkuu wa TAKUKURU, Mkoa wa Morogoro Emmanuel Kiyabo,
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU, Mkoa wa Morogoro Emmanuel Kiyabo, amesema hali hiyo ndio inayosababisha migogoro ya ardhi kuendelea kushika kasi katika mkoa huo.
Aidha Bw. Kiyabo, amewataka viongozi wa vijiji kuacha mara moja tamaa ya kupokea fedha za wafugaji kuwapatia maeneo ya malisho kwenye mashamba ya wakulima hali inayowapelekea wananchi hao kuanzisha migogoro mikubwa.
Katika hatua nyingine Kiyabo, amesema kuwa taasisi hiyo imeokoa zaidi ya shilingi milioni 27 fedha za miradi ya maendeleo zilizokuwa mikononi mwa watuhumiwa zikiwemo fedha za mradi wa kuweka alama za barabarani manispaa ya Morogoro.
Kufuatia kukithiri kwa matukio ya viongozi wa serikali pamoja na baadhi ya wabunge kukumbwa na kashfa za rushwa wakazi wa mji wa morogoro wameeleza kitendo hicho kimeondoa imani kwa wananchi kuwaamini wabunge wao na wameziomba mamlaka husika kuwashugulikia kikamilifu wabunge wanaokumbwa na kashfa hizo.