Friday , 24th Jul , 2015

HATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jiji la Mbeya wamepata mgombea wa kiti cha ubunge Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu” aliyeibuka kidedea baada ya kura zaidi ya 300 na kuwabwaga wananchama wenzake.

Mgombea wa kiti cha ubunge Jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi “Sugu”

Akitangaza matokeo katika mkutano mkuu maalum kwa ajili ya uchaguzi msimamizi wa uchaguzi Frank Nyalusi, ametaja idadi ya wapiga kura ni 455 na kura zilizoharibika ni tano.

Nyalusi ameendelea kutaja matokeo hayo ambayo wanachama wameelezea kuyakubali licha ya kuwepo minong’ono ya hapa na pale.

Awali akitangaza matokeo ya nafasi ya viti maalum ya baraza la wanawake Chadema (BAWACHA), msimamizi huyo huku akiwahakikishia kuwa uchaguzi ulikwenda bila mizengwe.

Wakizungumza na chombo hiki nje ya mkutano huo baadhi ya wanachama Jailos Peter Suzan Julius na Jiofray Mwandenga wamepongeza uchaguzi huo kuwa ulikuwa huru na haki na wametumia demokrasia yao.