Tuesday , 31st May , 2016

Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili nchini Tanzania (SHIVYATIATA) limesema kuwa kuendelea kwa vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kunaathiri utendaji kazi wao kwani jamii inawanahusisha moja kwa moja na mauaji hayo.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo Katibu Mkuu wa SHIVYATIATA Bw. Othman Shem amesema kuwa wao wanajiandaa kufanya mkutano mkubwa utakaojadili namna nzuri ya kukabiliana na maujia hayo huku wakiendelea kupeana elimu.

Katika hatua nyingine SHIVYATIATA hivi sasa wamepiga marufuku shughuli za kupiga ramli ziklizokuwa zinafanywa na baadhi ya waganga wa tiba asili kwani ramli zimeonekana kuleta migogoro mingi na mauaji kwenye jamii.