Monday , 25th Jan , 2016

Takwimu za ndoa za utotoni duniani zinaonyesha kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na ndoa za utotoni ambapo watoto wa kike wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Rebecca Gyumi

Takwimu za ndoa za utotoni duniani zinaonyesha kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na ndoa za utotoni ambapo watoto wa kike wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Mwanaharakati wa haki za binadamu anayetetea haki za watoto wa kike, Rebeca Gyumi amefungua shauri katika mahakama kuu ya Tanzania kupinga vipengele viwili vya sheria ya ndoa vinavyotoa mwanya wa mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa kibali cha mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi .

Vipengele vinavyopingwa katika shauri hilo ni kifungu cha 13 na 14 vya sheia ya ndoa vinavyopingana na ibara ya 12,13 na 14 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 vinavyotoa haki ya usawa mbele ya sheria, kutobaguliwa kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa kujieleza.

Akiongea mara baada ya kufungua shauri hilo wakili Jebra Kambole amesema kifungu hicho cha 17 kinatoa ruhusa ya mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 15 kwa kuolewa.

Mwanaharakati Rebeca Gyumi anasema ameamua kufungua shauri hilo ili kuondokana na ongezeko la ndoa za utotoni lililoshamiri katika mikoa ya Kaskazini hususani katika mikoa ya Shinyanga na Dodoma.

Baadhi ya wazazi jijini Dar esw salaam wakitoa maoni yao kuhusiana na tatizo hilo, wamesema hatua za makusudi zinahitajika ili kuondokana na mimba za utotoni.

Pamoja na utoaji wa elimu kwa jamii, vikundi vya dini na kupinga mila na desturi zinazochangia kuendelea kwa ndoa za utotoni ni muhimu kutokomeza ndoa za utotoni.