Umati mkubwa wa wananchi wa Zanzibar umejitokeza kumpokea Rais wa Ujerumani Joachim Gauck huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa nchi kutoka nje ya nchi kuwasili kwa usafiri wa baharini na kutembea kwa miguu hadi hotelini alipofikia kwa mapumziko.
Rais Joachim Gauck aliwasili kwa boti iendayo kwa kasi ya Kiliamnjaro na kupokewa na mwenyeji wake Dr Ali Mohamed Shein Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ambapo akiwa eneo hilo la bandari ya Zanzibar aliweza kupigiwa mizinga 21 iliyopigwa na kikosi cha JWTZ na baadaye kukagua gwaride la jeshi hilo.
Baadaye alitoka nje ya bandari na kupokolewa na wananchi na vikundi vya ngoma na ndipo baadaye akaanza msafara wa kiasi ya kilometa moja kuelekea hotelini kwa miguu huku akiangalia mandhari ya mji mkongwe na kusalimiana na waannchi.
Rais huyo wa Ujerumani alielekea ikulu na kuonana na Rais wa Zanzibar na ujumbe wa seriklai ya kitaifa ambapo viongozi hao walizungumzia ushiriki wa nchi hizi mbili za Zanzibar na Ujerumani ambapo Dr Shein amesema Zanzibar ina urafiki wa miaka mingi na kuishukuru Ujeruamni kwa misaada mbalimbali ikiwemo ya kijamii, bajeti na nishati.
Kwa upande wake Rais Joachim amesema amefurahishwa na umoja wa wazanzibari aliouona na kufurahishwa na wazanzibari kutatua matatizo yao wenyewe na kuona watu wote wa dini tofauti wako pamoja.
Rais Joachim alipata fursa ya kuonana na viongozo wa dini wa Zanzibar wakiwemo wa kiisilamu na madhehebu mbalimbali ya kikristo ambapo suala la amani na tafauti za dini ndiyo zilizokuwa agenda kuu.
Hata hivyo ujio wa kiongozi huyo kwa njia ya bandari na kutembea kwa miguu umeleta gumzo kubwa hapa Zanzibar huku wananchi wakionekana kuwa na mshangao wa hatua za makusudi za kung'arisha mji mkongwe na usafi wa hali ya juu hali inayoashiria kuwa wazanzibari wanaweza kuijenga nchi yao.