Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akijibu moja ya maswali yaliyoelekezwa kwenye wizara yake katika kipindi cha maswali na majibu
Akitoa taarifa leo Bungeni Mjini Dodoma Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage amesema kuwa pia serikali itafuatilia kumpata anayesambaza ujumbe wa kuwa kutakuwa na upungufu wa mafuta kwa siku mbili nchini Tanzania.
Mh. Mwijage amesema kuwa serikali inajua takwimu za mafuta yaliyopo ambapo amesema mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya upungufu huo wa mafuta ingawa serikali inafuatilia kwa ukaribu juu ya suala hilo.
Ameongeza kuwa Sheria za EWURA zinaruhusu kumfungia mmiliki yoyote wa biashara ya mafuta atakaye kataa kuyauza na kusema kuwa leseni za usambazaji na biashara hiyo ni mali ya serikali.