Sunday , 3rd Dec , 2017

Serikali imesema Taifa linahitaji vijana wenye maadili mema na wenye hofu ya Mungu watakaoliwezesha taifa kufikia mageuzi ya kiuchumi na kijamii ambayo kila mtu katika jamii amekuwa akiyahitaji.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati kongamano na kufungua mwaka wa mafunzo kwa vijana, kongamano lililotanguliwa na kambi maalumu ya vijana.

Profesa Ndalichako amesema katika wadhifa wake wa Waziri wa Elimu, anatamani kuona siku moja vijana wote nchini wanakuwa na maadili mema na kwamba hilo linawezekana iwapo kila mtu katika jamii anashiriki kuwandaa vijana kuwa raia wema na kwamba ni wajibu kwa vijana wenyewe kuwa tayari kupokea mafundisho kutoka kwa walezi wao.