Moja ya ghala lilisheheni sukari za wazalishaji wa Sukari wa Kilombero Mkoani Morogoro nchini Tanzania.
Wakizungumza mbele ya Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara mkoani Humo wakulima hao wamesema kuwa kwa hali ilivyosasa itawalazimu kufunga viwanda vyao kutokana na Maghala yao kujaa Sukari ambayo mpaka sasa hawajapata sehemu kwa kuzipeleka.
Kwa upande wao Wafanyabiashara wakubwa wa Sukari nchini Tanzania wamesema kuwa wao wako tayari kuweza kununua sukari za wazalishaji wa ndani huku wakipinga vikali wazalishaji hao kupewa jukumu la wao ndio kuwa wanaagiza sukari hizo.
Wafanyabiashara hao wamesema kilio hicho cha wazalishaji hakina ukweli wowote kwa sababu wameshanunua tani nyingi za sukari katika maghala yao na bado wapo katika mchakato wa kuweza kuzinunua sukari zilizopo.