Friday , 17th Oct , 2014

Serikali ya Tanzania imeshauriwa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa vijana juu ya athari mbaya zinazoweza kujitokeza ikiwemo kupoteza maisha au kupata majeraha mabaya endapo atalisogelea lori la mafuta mara tu baada ya kupata ajali na kupinduka.

Wananchi wakishuudia ajali ya Lori la mafuta Mbagala Jijini Dar es Salaam.

Ushauri huo umetolewa jana na wakazi wa jiji la Dar es salaam kufuatia kuwepo kwa matukio ya mara kwa mara ya wananchi kuwa na tabia ya kulifuata lori la mafuta mara baada ya kupata ajali kwa lengo la kuchukua mafuta.

Aidha wakazi hao wa jiji wamesema umasikini unaochangiwa na kipato duni miongoni mwa vijana wengi wa jijini Dar es salaam imekuwa ni chanzo kwa vijana hao kujiingiza katika majanga yasiyo ya lazima.

Hayo yanajiri baada ya hivi karibu ajali ya Lori la mafuta kuanguka na maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam, ambapo wananchi wa eneo wataka kunufaika na ajali hiyo ndipo lilipolipuka na kuuwa watu saba na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya