Tuesday , 20th Oct , 2015

Serikali ijayo imetakiwa kupitia upya mfumo wa elimu, kwa kurejesha mchujo kwa wanafunzi wanaofanya vibaya kitaaluma, ili kwenda sambamba na soko la ulimwengu linalohitaji zaidi ushindani na uhakika wa kumiliki uchumi.

Mwenyekiti wa shule na vyuo visivyo vya kiserikali nchini,Mrinde Mzava,

Mwenyekiti wa shule na vyuo visivyo vya kiserikali nchini, Mrinde Mzava, amesema kitendo cha serikali ya sasa kuondoa mchujo kwa wanafunzi wanaofanya vibaya kitaaluma, ni tatizo kubwa na kuongeza kuwa wazazi na serikali watalaumiwa kwa kushindwa kuwapatia watoto elimu bora.

Aidha Mzava ameshauri mpango wowote unaohusu marekebisho ya elimu ni vyema yakashirikisha wadau kwanza kwani dunia ya sasa kuwekeza kwa mtoto kwenye elimu ni jambo muhimu linalopaswa kupewa kipaumbele.

Kwa upande wao wadau wa elimu, wameshauri serikali ijayo kupitia upya mitaala ya elimu kwa kuachana na historia ya kuendeleza elimu ya ukoloni, kwa kuhakikisha elimu inayotolewa inalenga kumpeleka mwanafunzi kwenye kazi fulani,ikiwemo kupenyezwa kwa masomo ya ujasiriamali, kilimo bora na ufundi.