Saturday , 2nd May , 2015

Gavana wa Benki ya Tanzania BOT Prof. Beno Ndullu ameitaka serikali kutokuwa na matumizi yatakayosababisha kumaliza akiba ya fedha zilizopo kwa kuwa kunaweza kusababisha nchi kushindwa kukopesheka.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BOT Bw. Beno Ndulu

Gavana huyo wa Benki kuu ya Tanzania ametoa ushauri huo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge wa kamati ya bunge ya Viwanda na Biashara.

Amesema ni vema serfikali ikawa na matumizi yanayoweza kuwa na akiba ambayo hata pale panapohitajika fedha za kukopa kutoka nje ya nchi inaweza kupata fedha hizo bila ya kuwepo kwa vipingamizi.