Friday , 19th Feb , 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema tangu serikali ya awamu ya tano ianze kusimamia upatikanaji wa mapato bandarini imefanikiwa kukusanya shilingi bilion 1.9.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa

Prof. Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifanya mahojiano maalum na East Africa Radio na kuongeza kuwa na serikali inategemea kukusanya malipo zaidi kwa kontena elfu 11 zilizopotea bandarini na magari 2019 ambazo pesa hizo zikilipwa watakusanya takribani shilingi bilion 43 za kitanzania.

Aidha Prof. Mbarawa amesema kuwa waliokwepa kulipa kodi bandarini wameanza kuwafikisha mahakamani na wengine wamewafungia biashara zao sambamba na kuwasimamisha kazi wafanyakazi 15 wa bandari ambao walisaidia wateja au makampuni katika ukwepaji wa kodi.

Waziri huyo ameongeza kuwa kwa sasa bandari imejiwekea malengo ya kukusanya takribani trilion 1 kwa mwaka na tayari serikali imeunda tume yakuchunguza malipo yote yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika kupitia bandari hiyo.