Mkurugenzi wa Habari kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zamaradi Kawawa (kushoto) akiwa na Meneja Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji - TIC Bw. Daudi Riganda.
Taarifa hizo za The Economist, zimenukuliwa pia na gazeti moja la Kiswahili hapa nchini kwamba sera zinazotekelezwa na serikali ya rais Magufuli zimepunguza kiwango cha uwekezaji hususani kutoka nje.
Meneja Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji nchini TIC, Daudi Riganda, amesema hayo jijini Dar es Salaam leo na kwamba katika kipindi hicho, miradi yenye thamani ya takribani shilingi bilioni tisa imewekezwa nchini tofauti na miradi yenye thamani ya shilingi bilioni tano iliyowekezwa katika kipindi cha miezi sita iliyoishia Disemba mwaka jana.
Riganda amesema serikali kupitia Wizara ya Habari inakusudia kuiandikia serikali ya Uingereza juu ya habari hiyo aliyodai kuwa inalenga kuchafua sifa nzuri ya Tanzania kama sehemu bora ya uwekezaji duniani na kwamba isipokanushwa inaweza kuwatisha wafanyabiashara wanaolenga kuja kuwekeza nchini..
Katika hatua nyingine, Benki ya Barclays nchini imebuni mkakati wa kupunguza urasimu na usumbufu wakati wa kufungua akaunti katika matawi yake sehemu mbali mbali nchini ambapo huchukua muda usiozidi dakika ishirini kwa mteja kufungua akaunti yake katika benki hiyo.
Mkuu wa Mtandao wa Wateja wa benki hiyo Bw. Emmanuel Katuma amesema utaratibu huo unaendana na maboresho ya utoaji huduma wa benki hiyo hasa kwa kutumia kukua kwa teknolojia na utahusisha wateja wanaofungua akaunti za shilingi na sio wale wa fedha za kigeni.
Mkuu wa Shughuli za Kibenki Bi. Msungu Mwilingo amesema kupitia ubunifu huo, wateja hawatalazimika kubeba msururu wa vielelezo kama vile picha za passport size ambazo kulingana na maboresho hayo, mteja atapigwa picha akiwa anahudumiwa na taarifa zake kuchukuliwa na kuhifadhiwa moja kwa moja kwenye kompyuta.