Tuesday , 1st Dec , 2015

Serikali imefuta posho zote za vikao vya kamati za bunge na posho za vikao vya bodi za mashirika na taasisi za umma ili kuhakikisha taasisi za serikali hazitumii vibaya fedha za serikali.

Msajili wa hazina Lawrence Mafuru

Akizungumza na Wakurugezi wa Taasisi za Serikali na wajumbe wa bodi jana Jijini Dar es Salaam msajili wa hazina Lawrence Mafuru amesema kuwa taasisi na mashirika ya serikali yanatakiwa kuwa chachu ya Uzalishaji utakaosaidia kukua kwa pato la Taifa.

Msajili huyo wa Hazina amesema kuwa kuna taasisi na mashirika mengine ya Umma yamekua mzigo kwa serikali kutokana na kutokuwa na msaada wa uzalishaji kwa serikali zaidi ya kuongeza matumizi na kutoa kuwa na tija kwa taifa.

Mafuru ameongeza kuwa serikali imeamuru kufutwa kwa posho za vikao vya bodi na badala yake wajumbe walipwe ada yao ya kuwa wajumbe na kukaa vikao vvinne tu kwa mwaka ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Aidha Mafuru pia ameagiza wakurugenzi na watendaji wakuu wa taaasisi wasiingiliwe katika utendaji wao wa kazi na Mawaziri na kila mmoja afanye kazi kwa kuzingatia nafasi yake.