Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Maafa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho,
Akizungumza na mkoani humo baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wahanga hao Bi. Naima amewashukuru watu wote walioguswa na kutoa msaada kwa waathrika hao wa mafuriko na kusema taasisi nyingine ziendelee kuwasadia wahanga hao.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa suala la maafa linapotokea mkoa husika unatakiwa kutumia rasimali zao kwanza katika kuwaokoa waliokumbwa na majanga kabla ya kuhitaji msaada zaidi kutoka serikalini na kusema kuwa kwa mkoa wa Iringa wamejitahidi kufanya hivyo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Wanguvu, amewashukuru wadau mbalimbali ambao wameendelea kutoka misaada mbalimbali kwa waliokumbwa na maafa na kusema kuwa zoezi la kuwaokoa waathirika wengine linaweza kukamilika siku mbili zijazo.