Tuesday , 23rd Feb , 2016

Serikali imeandaa mpango mkuu wa sekta ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi utakaoongoza upangaji na utekelezaji wa mikakati ya sekta ya mifugo ili kuinua kipato kinachotoka na mifugo na mazao yake.

Naibu waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mhe.William Tate Ole Nasha

Hayo yamesemwa leo jijini na Naibu waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe.William Tate Ole Nasha kwenye mkutano wa utayarishaji wa mpango mkuu wa sekta ya mifugo, uvuvi na umwagiliaji na kuongeza kuwa mpango huo utatokana na uchambuzi wa hali halisi ya sekta, rasilimali zilizopo kwenye kanda mbalimbali za uzalishaji nchini.

Aidha ameongeza kuwa mpango huo pia utajumuisha viwango vya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya mifugo sambamba na kuchambua vikwazo vya uzalishaji mkubwa wa kibiashara vinavyowakumbwa wakulima na wavigaji

Mhe. Ole Nasha ameongeza kuwa umuhimu wa mpango mkuu ni kuchangia katika kuondoa umaskini wa wafugaji, wafanyabiashara wa mifugo na wasindikizaji wa mazao na kuboresha uzalishaji wa mifugo na kuiendeleza sekta ya mifugo iweze kuchangia zaidi kwenye pato la kaya na taifa.

Kwa upande wa washiriki wa mkutano huo ambao ni wadau wa sekta ya kilimo,uvuvi, mifugo na umwagiliaji wamesema kuwa mpango huo utaleta mapinduzi ya sekta ya mifugo kwa kuondoa umaskini, kuongeza usalama wa chakula, lishe na kipato