Saturday , 26th Jul , 2014

Serikali ya Tanzania imeifungia Hospitali ya IMTU kwa muda usiojulikana kutokana na kukutwa na makosa mbali mbali kufuatia ziara ya Mganga mkuu wa Hopsiitali ya Manispaa ya Kinondoni Daktari Gunini Kamba.

Hospitali ya IMTU Dar es salaam.

Mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondonu Daktari Gunini Kamba amesema uamuzi wa kuifungia Hospitali hiyo ulitolewa jana baada ya ziara shirikishi kati ya Manispaa na Wizara ya afya na Maendeleo ya jamii ya kukagua Hosptali hiyo iliyochukua saa Nne.

Katika Ziara hiyo Mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni aliongozana na timu ya wataalamu mbali mbali wakiwemio wanasheria na Madakitari. Alisema wakiwa katika ziara ya ukaguzi timu iligundua kuwepo kwa mapungufu mengi ukiwamo kutokuwa na kibali cha maabara kwa kipindi cha miaka mitatu.

Dk. Kamba, alisema upungufu mwingine ni uhaba wa watumishi wakiwemo wauguzi na tanuru la kuchomea taka za hospitali kutokuwapo hospitalini baada ya lile linalotumiwa sasa kutakiwa kulirekebisha. Alisema ziara hiyo iligundua kuwa tanuru hilo liliendelea kutumiwa na kukiuka maagizo yaliyotolewa na kuendelea kuharibu mazingira. Aidha, alisema hospitali hiyo pia imekiuka utaratibu kwa kumuweka Mfamasia ambaye hakusajiliwa na Manispaa.

Kadhalika dawa zilizokwisha muda wake hazikuondolewa kwenye chumba cha kuhifadhiwa dawa mpaka walipokwenda kwenye ukaguzi na kuzikuta bado zikiwa kwenye chumba.

Tags: