Friday , 12th Dec , 2014

Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa amewataka watanzania kutokatishwa tamaa na maneno yanayozungumzwa kwenye majukwaa ya kisiasa juu ya utendaji kazi wa serikali iliyoko madarakani.

Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa

Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa amewataka watanzania kutokatishwa tamaa na maneno yanayozungumzwa kwenye majukwaa ya kisiasa juu ya utendaji kazi wa serikali iliyoko madarakani, badala yake waipime kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na ahadi ilizotoa kwani licha ya changamoto zilizopo imefanya mambo mengi makubwa na yanayoonekaana.

Akizungumza katika mikutano ya kuwanadi wagombea wa uongozi wa serikali za mitaa na vijiji katika kata ya Majengo na Mto wa Mbu, wilayani Monduli Mh Lowassa amesema changamoto zilizopo zisiwe kigezo cha kuihukumu CCM wakati wa uchaguzi na kwamba kufanikiwa ama kutofanikiwa kunapimwa kwa vitendo na wala sio maneno.

Katika hatua nyingine Mh Lowassa ameishauri serikali kuangalia upya namna ya kukakabiliana na migogoro ya ardhi hasa kwa wananchi wanaoishi karibu na hifadhi za wanyamapori kwani inavyoonekana licha ya kuwepo kwa sheria nzuri utekelezaji wake unaelekea kuwajali zaidi wanyamapori badala ya wananchi.