Monday , 24th Nov , 2014

Mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania yanayojishughulisha na masuala ya kisheria na maendeleo nchini Tanzania yamesema kuwa serikali imejitahidi kuungana nao katika kuhamasisha kutokomezwa ukatili wa kijinsia na kusaidia kupungua

Mkurugenzi wa WILDAF, Dkt. Judith Odunga.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Mipango wa Shirika la Wanawake katika Maendeleo na Sheria (WILDAF) Anna Kulaya wakati shirika hilo likitangaza kuanza kwa maadhimisho ya siku kumi na Sita za kupinga ukatili wa kijinsia.

Bi.Kulaya amesema ushirikiano uliopo miongoni mwa asasi mbalimbali pamoja na serikali umesaidia kupunguza kiwango cha unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ili ya kuwepo kwa changamoto kadhaa.

Amesema kuwa Vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vimepungua Tangu kuanza kwa maadhimisho ya siku hizo kumi na Sita na utafiti unaonesha watoto na wanawake ndio waathirika wakubwa wa unyanyasaji wa Kijinsia.