Tuesday , 24th Jun , 2014

Serikali imesema iko katika mkakati wa kukuza elimu ya vyuo vya ufundi ili kukuza uchumi na kupunguza kasi ya vijana kukimbilia mijini ambako ndiko wanakodhani kuna fursa za ajira.

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kukuza uchumi ulioandaliwa na Benki ya Dunia Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amesema vijana wengi wanakimbilia mjini wakiwa hawana ujuzi wowote.

Mhe. Pinda amekiri kuwa elimu ya sasa haimkomboi kijana kiuchumi hivyo serikali imeamua kupanua vyuo vya ufundi ili iwakomboe wananchi hasa vijana wanawake katika kujitegemeza kiuchumi.