Tuesday , 7th Jun , 2016

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa amesema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 173 zimetengwa kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya Iringa -Igawa yenye urefu wa kilomita 137.9

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa amesema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 173 zimetengwa kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya Iringa -Igawa yenye urefu wa kilomita 137.9.

Akiongea wakati akikagua barabara hiyo Prof Mbarawa amesema kuwa kwa muda mrefu barabara hiyo imelalamikiwa kusababisha ajali nyingi hivyo serikali imeamua kupanua kutoka mita 8 za hapo awali mpaka kufikia mita 12 ili kuwezesha magari kupishana bila kusababisha ajali.

Barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya TANZAM inayounganisha nchi yaTanzania na Zambia pamoja na Malawi itakuwa kiungo muhimu cha kukuza uchumi kwa kurahisisha biashara kati yaTanzania na nchi hizo mbili hivyo ni jumkumu la watanzania kuitunza ili iwaletee maendeleo.

Aidha amemtaka mkandarasi wa barabara hiyo ambaye ni China Civic Engeneering Construction Cooperation (CCECC) kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyo kwenye mkataba kwani kujenga barabara chini ya kiwango kutawafanya wasiruhusiwe kujenga barabara yoyote nchini Tanzania.