Tuesday , 17th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imeahidi kudhibiti upungufu unaosababisha watumishi wengi wa serikali kutopewa mishahara na stahiki zao mara wanapopanda daraja na kupandishwa vyeo na kulazimishwa kukubali cheo kabla ya kupanda kwa mshahara.

Waziri wa nchi ofis ya rais anayeshughulikia Utumishi, Bi. Celina Kombani

Akijibu swali la Mhe. Clara Diana Mwatuka katika kipindi cha maswali na Majibu Bungeni mjini Dodoma, aliyetaka kufahamu utaratibu unaofuatwa ili mtumishi aweze kupewa stahiki zao mara baada ya kupandishwa cheo, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejiment na Utumishi wa Umma Celina Kombani amesema serikali imeweka mfumo wa taarifa za Utumishi na Mishahara

Mhe Kombani ameongeza kuwa mara mtumishi anapopanda daraja au kupandishwa cheo, huingizwa kwenye mfumo huo ambao ulianzishwa mwaka 2012 hata kabla ya mwisho wa mwezi, ili apatiwe stahiki zake mara moja.