
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa - TAMISEMI, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema tayari serikali imekuwa ikitoa fedha shilingi milioni hamsini kwa kila shule kwa ajili ya ukarabati unaohusisha shule takribani mia tano na arobaini na saba.
Waziri Majaliwa amesema zoezi la ukarabati huo linahusisha kuongeza idadi ya madarasa, baada ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa miaka mingi kubomoka kiasi cha kufanya shule hizo kuonekana kama majengo ya kale.
Ameongeza kuwa mpaka sasa serikali imeshatoa awamu tano ya fedha hizo ambapo kila shule imeshapata wastani wa shilingi milioni mia mbili na hamsini na kwamba zoezi la ukarabati huo ni endelevu kutegemea na fedha zinazotengwa katika bajeti.