Msitu wa Sao Hill
Akizungumza na East Africa Radio baada ya kufungua rasmi mradi wa Panda miti kibiashara Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mahmood Mgimwa amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na serikali ya Finland inatarajia kufufua kilicho kuwa chuo cha misitu cha sao hill mkoani Iringa kwa lengo la kutoa elimu ya kulima kibiashara.
Amesema kuwa serikali imeona umuhiumu wa kuwapa elimu ya utunzaji wa miti na kuhakikisha taifa rinanufaika na kilimo kinachofanyika katika Kanda hiyo ya Nyanda za Juu Kusini na kuwa chuo hicho kitafungulkiwa mwezi Januari mwaka ujao.
Kwa upande wa ke Mwakilishi wa Barozi wa Finland hapa Nchini Mikko alisema kuwa serikali yake inanufaika na kilimo cha miti na kuwa uchumi wanchi yao unategemea kilimo cha miti hiyo imani yake ni Tanzania kunufaika na kilimo hicho ambacho wananchi wake wanafundishwa kulima kibiashara.