Friday , 8th Jan , 2016

Wizara ya Mambo ya Ndani Nchini Tanzania imesema kuwa jeshi la zimamoto litahakikisha vifaa vya kuzimia moto vinapatikana ili kusaidia katika uokoaji mara moto unapotokea.

Wizara ya Mambo ya Ndani Nchini Tanzania imesema kuwa jeshi la zimamoto serikali itahakikisha vifaa vya kuzimia moto vinapatikana ili kusaidia katika uokoaji mara moto unapotokea.

Akitembelea makao makuu ya Jeshi la zima moto na Uokoaji jijini Dar es salaam na kukutana na watendaji wa jeshi hilo Waziri ya Mambo ya Ndani Charles Kitwanga amesema uwepo wa magari matano pekee ya kuzima moto na uokozi katika mkoa wote wa Dar es salaam pamoja na gari kubwa moja la kisasa lenye uwezo wa kuzima moto hadi gorofa ya 18 wakati kuna majengo yenye gorofa hadi 35 hayakidhi uhitaji wa huduma za uokoaji.

Waziri kitwanga ameongeza kuwa atajitahidi kuwapigania ili bajeti ya jeshi hilo iongezeke ili kurahisisha kazi yao muhimu ya kuokoa mali na uhai wa watanzania ili kuwafikia wananchi wanaohitaji huduma za jeshi hilo kwa wakati pamoja na kutafuta eneo lingine la kuhifadhia vifaa .

Waziri kitwanga amewataka wananchi kulipisha gari la zimamoto wanapokutana nalo katika barabara ili kuwahi kuzima moto.

Kwa upande wake kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam wa Jeshi hilo, Jesward Ikonko amesema kuwa uchache wa vitendea kazi, bajeti ndogo, uhaba wa maji, ukosefu wa barabara maalum kwa magari ya zimamoto ni miongoni mwa changamoto kubwa katika jeshi hilo.