Wednesday , 4th May , 2016

Serikali imesema kuwa inafanyia mabadiliko mpango wa miaka mitano wa ujenzi na ukarabati wa mahakama nchini ikiwa ni pamoja na kurekebisha maslahi ya Mahakimu na wanasheria ili wafanye kazi hiyo kwa weledi zaidi.

Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe

Akijibu swali lililoelekezwa katika Wizara ya Katiba na Sheria juu ya Mpango wa serikali kuboresha na kutengeneza mahakama kwa ajili ya kupunguza mlolongo wa mashauri waziri wa wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema bajeti yake tayari ipo kwa ajili ya shughuli hiyo.

Dk. Mwakyembe amesema katika bajeti ya Mwaka 2015/2016, serikali imetenga shilingi bilioni 12.3 za miradi ya maendeleo ambazo ni sawa ma asilimia 100 ambapo fedha fedha hizo zimepangwa kutengeneza mahakama 12 nchini.

Dkt. Mwakyembe amesema ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa inawalipa vizuri maafisa wa mahakama kwa mujibu wa sheria huku akisema kuwa katika suala la ulipaji majaji Tanzania ni moja kati nchi zilizopiga hatua katika kuwalipa majaji.