Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, CCM, Abdulrahman Kinana
Chama Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya waliobinafshiwa viwanda nchini sanjali na kunyang'anywa viwanda hivyo na kurudishwa kuwa mali ya umma.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa, Bw. Abrahmani Kinana,inakuja mara baada ya kutembelea na kujionea,mlundikano wa korosho na msururu wa magari ya kisubili kupakuliwa,huku moja ya kiwanda cha kubangua korosho na ufuta kikigeuzwa ghala la kuifadhia vifaa vya kusambazaia umeme.
Bw. Kinana akihutubia kwenye mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nachingwea Mkoani Lindi,ameitaka serikali kuwawajibisha viongozi au watumishi wa umma,ambapo amesema serikali haipaswi kuogopa watu wachache hasa wenye fedha na kuwacha mamilioni ya watanzania waliowaweka madarakani wakitaabika.
Kwa upande wake Katibu mwenezi wa Chama hicho Ndugu Nape Nnauye, amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kufanya maamuzi sahihi kwa kukiweka chama hicho madarakani kuanzia ngazi za chini ili kuweza kumalizia miradi waliyoianzisha au ina tija katika maendeleo yao ya baadae.