Monday , 15th Sep , 2014

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Josefu Msukuma amemuomba Naibu waziri wa Nishati na madini kuwachukulia hatua wawekezaji wanaopora maeneo yanayotengwa kwa wachimbaji wadogo wadogo.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Maselle.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti huyo mbele ya Naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele wakati akikabidhi eneo la kuchimba dhahabu kwa wachimbaji wadogo wadogo lililoko katika kijiji cha Lwamgasa Wilayani Geita - Mkoani humo.

Msukuma amesema kuwa kumekuwa watu ambao wanaopora maenaeo ya wachimabaji wadogo wadogo kwa kuwalazimisha kuingia ubia na mwishoe kuwadhulu na kuwafukuza ambapo huanza kuhangaika.

Ameongeza kuwa migogoro ya wachimbaji wakubwa na wadogo haiwezi kuisha kama wachimbaji wakubwa hawataacha kuwadhulumu maeneo yao hivyo kumuomba naibu waziri kuwachukulia hatua kali wote waliopora maeneo yaliyotengwa kwa wachimbaji wadogo wadogo na kujimilikisha wao.

Naye Naibu waziri wa nishati na madini akiongea na wananchi wakati wa kuzindua mgodi huo aliishukuru benki ya dunia na Mgodi wa GGM kwa kukubali kutoa pesa nyingi na vifaa kwa kuwasaidia wananchi hao mara baada ya kutambua mahusiano mazuri yaliopo kati ya mgodi na Serikali.