Saturday , 12th Nov , 2016

Aliyekuwa Spika wa Bunge la 9 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samuel John Sitta, amezikwa leo nyumbni kwao Urambo mkoani Tabora, kwenye makaburi ya familia.

Mazishi hayo yaliyoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kdini, kisiasa wabunge na mamia ya wakazi wa mji wa Urambo, yamefanyika mchana huu huku yakiacha mji wa Tabora na majoniz makubwa ya kumpoteza mtoto wao, baba yao na Kiongozi wao.

Akizungumza kwenye ibada ya mwisho ya kumuaga Mh. Samuel Sitta, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mh. SItta ana mchano mkubwa kwenye taifa hili kutokana na utumishi wake uliotuka wa muda mrefu, huku akiwataka watanzania kumuenzi Mh. Sitta kwa yale aliyoyafanya na kuyaishi, wakati wa uhai wake, na kwa upande wake ataendelea kumkumbuka kwa alivyomfundisha jinsi ya kuwa kiongozi bora, na kuheshimu kila mmoja.

Ibada ya mazishi iliongozwa na viongozi mbali mbali wa dini akiwemo Askofu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex malasusa, katika viwanja vya shule ya msingi Urambo Tabora.

Mh. Samuel John Sitta alizaliwa mwaka mwaka 1942 Urambo mkani Tabora, na amefariki tarehe 7 Novemba 2016, huku akiwa amepitia nyadhifa mbali mbali serikalini ikiwemo Spika wa Bunge la Tanzania katika Bunge la 9, waziri wa wizara mbali mbali na mwanachama wa CC.