Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu amesema rushwa, ubadhirifu na ufisadi nchini vimechangia kuzorotesha utoaji haki na kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha umasikini nchini.
Akiongea leo katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani, yalifanyika Mhe. Samia Hassan amesema serikali ya awamu ya tano itahakikisha inasimamia utoaji wa haki kwa kuimarisha maadili kwa watumishi wa umma pamoja na kupambana na kuongezeka kwa imani za kishirikiana zinazochangia kuongezeka kwa mauaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawakla Bora nchini Tanzania, Tom Nyanduga amesema kumekuwepo na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini katika matukio mbalimbali ya wananchi kujichukulia sheria mikononi, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na mauaji ya vikongwe kutokana na imani za kishirikina.