Mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMA Hashim Rungwe amesema kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya Mahakama nchini iliingilia uhuru wa mahakama.
Akielezea utata uliojitokeza katika hotuba hiyo Rungwe amesema hotuba hiyo ilionekana kama kuifundisha mahakama wajibu wake jambo ambalo lina utata katika uongozi wa kisheria lakini hata hivyo Rungwe ameielezea hotuba hiyo kuwa itaongeza uwajibikaji katika mahakama na haki kupatikana kwa wakati.
Wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama Alhamisi iliyopita, Rais Magufuli aliahidi kuipatia idara ya mahakama fedha kwa ajili ya kuendesha shuhguli za mahakama na kuitaka mahakama hiyo kuharakisha kusikiliza kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kesi za watuhumiwa wa kukwepa kulipa kodi.