Saturday , 21st Jun , 2014

Wakala wa usajili, Ufilisi, na udhamini nchini Tanzania RITA imewatahadharisha wananchi juu ya kuwepo kwa watu wachache wanaowadanganya wananchi kwa kutaka kuwatengenezea vyeti vya kuzaliwa pasipo kufuata utaratibu wa RITA.

Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alipokuwa akizindua vyeti vipya vya kuzaliwa mwezi wa kumi mwaka 2009

Wakala wa usajili, Ufilisi, na udhamini nchini Tanzania RITA imewatahadharisha wananchi juu ya kuwepo kwa watu wachache wanaowadanganya wananchi kwa kutaka kuwatengenezea vyeti vya kuzaliwa pasipo kufuata utaratibu wa RITA.

Tahadhari hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Afisa habari wa RITA Bw. Jafery Malema wakati alipokuwa akizungumza na East Africa Radio ambapo amewataka wananchi wanaohitaji vyeti hivyo kufika ofisi za RITA zilizopo wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam badala ya kutumia njia za panya.

Jafery amesema kutokana na kuwepo kwa udanganyifu huo unaofanywa na watu wachache wananchi hawana budi kuchukua tahadhari ili kupeukana na usumbufu wanaoweza kuupata pale watakapohitajika vyeti halisia vya kuzaliwa.