
Mufti wa Tanzania (Wa pili kulia) akipokea ripoti ya uchunguzi wa mali za BAKWATA
Akizungumza wakati wa kumkabidhi ripoti hiyo, Mwenyekiti wa tume hiyo Sheikh Abubakari Khalid Hajj amesema kuwa ripoti hiyo imefanyika kwa muda wa miezi mitatu licha ya kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa muda.
Aidha amewambia wanahabari kuwa uchunguzi huo umehusisha ufuatiliaji wa mali za Bakwata katika Mkoa wa Dar es salaam pekee,ikiwemo majengo,viwanja, pamoja na kupitia mikataba mbalimbali ili kujiridhisha kama imefuata taratibu za kisheria.
Sheikh Abubakari Zuber
Akizungumza mbele ya wanahabari mara baadi ya kupokea ripoti hiyo Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber amesema kuwa ataipitia ripoti hiyo ili kujua yale yaliyobainishwa na tume yake, na kuahidi kuyafanyia kazi mapema iwezekanavyo.
Hata hivyo Mufti huyo ameiongezea muda wa miezi mitatu tume hiyo ambayo ina jumla ya wajumbe wanane kwa ajili ya kukamilisha kuandaa ripoti ya mkoa wa Dar es salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine kwani zoezi hilo litafanyika nchi nzima.