Tuesday , 26th May , 2015

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi ameunda tume huru ya watu 8 inayowashirikisha viongozi wa dini na serikali kwa ajili ya kuchunguza vurugu kubwa zilisababisha maandamano Mei 20, mwaka huu mjini Njombe.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa usalama mkuu wa mkoa wa Njombe Dk. Nchimbi amelaani vikali vurugu hizo zilizotokea kwenye hospitali ya mkoa ya Kibena na kusababisha hofu kwa wagonjwa pamoja na wananchi wengine.

Ameyasema hayo mara baada ya kufungua mafunzo ya kuhusu wakala wa vipimo mkoani humo yaliyowashirikisha viongozi wanawake, wenyeviti, makatibu na madiwani wa Chama cha Mapinduzi wilaya za Njombe ambayo imeandaliwa na naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr. Pindi Chana , mkuu wa mkoa wa Njombe , Dk. Nchimbi amesema binafsi vurugu hizo kubwa zimemsikitisha sana.

Dk. Nchimbi amesema ni tukio ambalo lilimsononesha, kumsikitisha na kulielezea kuwa lilikuwa siyo sehemu ya matumaini yake kwa wakazi wa mkoa wa Njombe.

Amesema mauaji yaliyotokea ni kitu ambacho wananchi wameshtushwa na yamewashangaza, lakini pia namna hatua zilivyochukuliwa wakati wa lile tukio halikuwa la kawaida.

Nchimbi amesema hajafurahishwa na tetesi zilizogaa mjini Njombe kuwa kuna vijana wanajiandaa kuja kuungana na wenzao mjini Njombe kwenda kulipiza kisasi kwa askari polisi kwa madai walihusika kuua raia.

Mei 20, mwaka huu vurugu kubwa zilizodumu kwa saa tisa katika mji wa Njombe zikianzia katika Hospitali ya mkoa ya Kibena, kufuatia wananchi kufanya maandamano makubwa wakidaiwa kupinga askari polisi kudaiwa kuua raia mmoja kwa kumpiga risasi na kujeruhi mwingine katika Mtaa wa Kambarage.

Askali huyo ambaye jina lake halija fahamika anadaiwa kumuua Basil Mwalongo mkazi wa Kambalage aliuwawa katika kilabu cha pombe.